Genesis 18:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abrahamu na Sara walikuwa wakongwe, naye Sara mambo ya kawaida ya wanawake yalikuwa yamekoma kitambo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ibrahimu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikuwa amepita umri wa kuzaa mtoto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abrahamu na Sara walikuwa wakongwe, naye Sara mambo ya kawaida ya wanawake yalikuwa yamekoma kitambo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Abrahamu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikwishakoma katika desturi ya wanawake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ibrahimu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Abrahamu na Sara walikuwa wazee wenye umri mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abrahamu na Sara walikuwa wakongwe, naye Sara mambo ya kawaida ya wanawake yalikuwa yamekoma kitambo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Aburahamu na Sara walikuwa wazee wenye siku nyingi, naye Sara alikuwa amekoma kupatwa na yale mambo ya kike.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abrahamu na Sara walikuwa wazee sana, naye Sara hangeweza tena kuzaa.