Genesis 18:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Sara, akiwa na hofu, akakana akisema, “Sikucheka!” Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Sivyo! Kucheka, ulicheka.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sara akaogopa, hivyo akadanganya na kusema, “Mimi sikucheka.” Lakini Mwenyezi Mungu akasema, “Ndiyo, ulicheka!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Sara, akiwa na hofu, akakana akisema, “Sikucheka!” Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Sivyo! Kucheka, ulicheka.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka.” Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka.” Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sara akakana, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo! Umecheka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Sara, akiwa na hofu, akakana akisema, “Sikucheka!” Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Sivyo! Kucheka, ulicheka.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Sara akakana kwamba: Sikucheka, kwani aliogopa; naye akasema: Sivyo, umecheka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Sara, akiwa na hofu, akakana akisema: “Sikucheka!” Yawe akamwambia: “Ndiyo, ulicheka!”