Genesis 18:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo wale watu wakaondoka, wakafika mahali walipoweza kuona mji wa Sodoma; naye Abrahamu akawasindikiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu hao waliposimama ili waondoke, walielekeza nyuso zao Sodoma, naye Ibrahimu akatembea nao ili awasindikize.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo wale watu wakaondoka, wakafika mahali walipoweza kuona mji wa Sodoma; naye Abrahamu akawasindikiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati watu hao waliposimama ili waondoke, walielekeza nyuso zao Sodoma, Abrahamu akawatoa kitambo kidogo ili awasindikize.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati watu hao waliposimama ili waondoke, walielekeza nyuso zao Sodoma, Ibrahimu akawatoa kitambo kidogo ili awasindikize.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Abrahamu akaenda pamoja nao awasindikize.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo wale watu wakaondoka, wakafika mahali walipoweza kuona mji wa Sodoma; naye Abrahamu akawasindikiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wale waume wakaondoka huko, wakajielekeza kwenda Sodomu, naye Aburahamu akaenda nao, awasindikize.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha wale watu wakaondoka, wakafika pahali walipoweza kuona muji wa Sodoma; naye Abrahamu akawasindikiza.