Genesis 18:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na alipoinua macho yake, akaona watu watatu wamesimama mbali kidogo mbele yake. Mara alipowaona, akapiga mbio kutoka mlangoni mwa hema lake, akaenda kuwalaki. Alipowafikia aliinama kwa heshima na kusema,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ibrahimu akainua macho, akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, akaharakisha kutoka ingilio la hema lake, akawalaki na kusujudu hadi chini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na alipoinua macho yake, akaona watu watatu wamesimama mbali kidogo mbele yake. Mara alipowaona, akapiga mbio kutoka mlangoni mwa hema lake, akaenda kuwalaki. Alipowafikia aliinama kwa heshima na kusema,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ibrahimu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka chini,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na alipoinua macho yake, akaona watu watatu wamesimama mbali kidogo mbele yake. Mara alipowaona, akapiga mbio kutoka mlangoni mwa hema lake, akaenda kuwalaki. Alipowafikia aliinama kwa heshima na kusema,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoyainua macho yake akaona watu watatu, wakisimama hapo, alipo; alipowaona akawapigia mbio na kuondoka hapo pa kuingia hemani, akawainamia chini,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipoinua macho yake, akaona watu watatu wakisimama mbali kidogo mbele yake. Mara tu alipowaona, akakimbia kutoka kwenye mulango wa hema yake, akakwenda kuwapokea. Alipowafikia akainama kwa heshima