Genesis 18:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutoka hapo, wale watu wakashika njia kuelekea Sodoma, lakini Mwenyezi-Mungu akawa amebaki, amesimama pamoja na Abrahamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi wale watu wakageuka, wakaelekea Sodoma, lakini Ibrahimu akabaki amesimama mbele za Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutoka hapo, wale watu wakashika njia kuelekea Sodoma, lakini Mwenyezi-Mungu akawa amebaki, amesimama pamoja na Abrahamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi wale watu wakageuka wakaenda kuelekea Sodoma, lakini Abrahamu akabaki amesimama mbele za BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi wale watu wakageuka wakaenda kuelekea Sodoma, lakini Ibrahimu akabaki amesimama mbele za bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Abrahamu alibaki amesimama mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutoka hapo, wale watu wakashika njia kuelekea Sodoma, lakini Mwenyezi-Mungu akawa amebaki, amesimama pamoja na Abrahamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wale watu wakageuka hapo kwenda Sodomu, lakini aburahamu akasalia hapo akisimama mbele ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutoka pale, wale watu wakashika njia kuelekea Sodoma, lakini Yawe akabaki, akisimama pamoja na Abrahamu.