Genesis 18:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sidhani kama utafanya hivyo! Kuwaua watu wema pamoja na waovu; wema kutendewa sawa na waovu! La, hasha! Hakimu wa dunia yote hataacha kutenda yaliyo sawa!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo: kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Liwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya haki?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sidhani kama utafanya hivyo! Kuwaua watu wema pamoja na waovu; wema kutendewa sawa na waovu! La, hasha! Hakimu wa dunia yote hataacha kutenda yaliyo sawa!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya lililo sawa?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya lililo sawa?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sidhani kama utafanya hivyo! Kuwaua watu wema pamoja na waovu; wema kutendewa sawa na waovu! La, hasha! Hakimu wa dunia yote hataacha kutenda yaliyo sawa!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jambo kama hilo halipasi kabisa, ulifanye, ukimwua mwongofu pamoja naye asiyekucha, mwongofu akiwa kwako kama mwingine asiyekucha. Hili halikupasi kabisa wewe utakayewaamua walimwengu wote, hayo si maamuzi, utakayoyaamua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sizani kama utafanya hivyo, kuwaua watu wa haki pamoja na waovu, kutendea watu wa haki sawa na waovu. Hapana, haiwezekani! Mwamuzi wa dunia yote hataacha kutenda mambo yanayokuwa sawa!”