Genesis 19:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale malaika wawili wakawasili mjini Sodoma jioni. Loti ambaye alikuwa ameketi penye lango la mji wa Sodoma, alipowaona, aliinuka kuwalaki, akainama kwa heshima,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wale wawili walifika Sodoma wakati wa jioni, naye Lutu alikuwa ameketi kwenye lango la mji. Alipowaona, alienda kuwalaki, akasujudu, uso wake ukagusa chini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale malaika wawili wakawasili mjini Sodoma jioni. Loti ambaye alikuwa ameketi penye lango la mji wa Sodoma, alipowaona, aliinuka kuwalaki, akainama kwa heshima,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wale wawili wakafika Sodoma wakati wa jioni, naye Loti alikuwa ameketi kwenye lango la mji. Wakati alipowaona, aliondoka kwenda kuwalaki na kuwasujudia hadi chini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wale wawili wakafika Sodoma wakati wa jioni, naye Lutu alikuwa ameketi kwenye lango la mji. Wakati alipowaona, aliondoka kwenda kuwalaki na kuwasujudia hadi chini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale malaika wawili wakawasili mjini Sodoma jioni. Loti ambaye alikuwa ameketi penye lango la mji wa Sodoma, alipowaona, aliinuka kuwalaki, akainama kwa heshima,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilipokuwa jioni, wale malaika wawili wakafika Sodomu, naye Loti alikuwa amekaa langoni huko Sodomu. Alipowaona Loti akainuka kuwaendea njiani, akawaangukia usoni chini,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wamalaika wawili wakafika katika muji wa Sodoma magaribi. Loti alikuwa ameketi kwenye mulango wa muji wa Sodoma. Alipowaona, akasimama kwenda kuwapokea, akainama kwa heshima.