Genesis 19:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale watu wawili wakamwambia Loti, “Je, una mtu mwingine hapa, pengine wana, mabinti, wachumba wa binti zako au watu wengine wa jamaa yako wanaoishi mjini humu? Watoe mahali hapa haraka,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wanaume wawili wakamwambia Lutu, “Una mtu mwingine yeyote hapa: wakwe, wana au binti, ama yeyote mwingine aliye wako katika mji huu? Waondoe hapa,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale watu wawili wakamwambia Loti, “Je, una mtu mwingine hapa, pengine wana, mabinti, wachumba wa binti zako au watu wengine wa jamaa yako wanaoishi mjini humu? Watoe mahali hapa haraka,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale watu wawili wakamwambia Loti, “Una mtu mwingine ye yote hapa, wakwe zako, wana au binti, ama ye yote mwingine aliye wako katika mji huu? Waondoe hapa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale watu wawili wakamwambia Lutu, “Una mtu mwingine yeyote hapa, wakwe zako, wana au binti, ama yeyote mwingine aliye wako katika mji huu? Waondoe hapa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Wakwe, wanao wa kiume au wa kike, na wowote ulio nao katika mji uwatoe katika mahali hapa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale watu wawili wakamwambia Loti, “Je, una mtu mwingine hapa, pengine wana, mabinti, wachumba wa binti zako au watu wengine wa jamaa yako wanaoishi mjini humu? Watoe mahali hapa haraka,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wale waume wakamwambia Loti: Kama unao ndugu, wakweo na wanao wa kiume na wa kike nao wo wote walio wako humu mjini, wachukue, utoke nao mahali hapa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale watu wawili wakamwambia Loti: “Uko na mutu mwingine hapa, pengine wana wako, wabinti, wachumba wa wabinti zako au watu wengine wa jamaa yako wanaoishi katika muji huu? Uwatoshe pahali hapa haraka,