Genesis 19:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Loti akawaendea wachumba wa binti zake, akawaambia, “Haraka! Tokeni mahali hapa, maana Mwenyezi-Mungu atauangamiza mji huu.” Lakini wao wakamwona kama mtu mcheshi tu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Lutu alitoka ili kuzungumza na wakwe wake waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa Mwenyezi Mungu yu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe wake walifikiri kwamba alikuwa akitania.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Loti akawaendea wachumba wa binti zake, akawaambia, “Haraka! Tokeni mahali hapa, maana Mwenyezi-Mungu atauangamiza mji huu.” Lakini wao wakamwona kama mtu mcheshi tu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Loti alitoka ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa BWANA yu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe zake walifikiri kwamba alikuwa akitania.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Lutu alitoka ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa bwana yu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe zake walifikiri kwamba alikuwa akitania.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Loti akawaendea wachumba wa binti zake, akawaambia, “Haraka! Tokeni mahali hapa, maana Mwenyezi-Mungu atauangamiza mji huu.” Lakini wao wakamwona kama mtu mcheshi tu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Loti alipotoka kusema na wakwewe waliowaoa wanawe wa kike, akawaambia: Inukeni, mtoke mahali hapa! Kwani Bwana ataungamiza mji huu. Lakini machoni pao wakwewe alikuwa kama mtu anayetaka kuwachekesha tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Loti akawaendea wachumba wa wabinti zake, akawaambia: “Haraka! Mutoke pahali hapa, maana Yawe atauangamiza muji huu.” Lakini wao wakamwona kama mutu mwenye kuchekesha tu.