Genesis 19:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulipokucha, malaika wakamhimiza Loti wakisema, “Amka, mchukue mkeo na hawa binti zako wawili msije mkaangamia wakati mji huu unapoadhibiwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulipopambazuka, malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, “Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walio huku, la sivyo utaangamizwa mji huu utakapoadhibiwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulipokucha, malaika wakamhimiza Loti wakisema, “Amka, mchukue mkeo na hawa binti zako wawili msije mkaangamia wakati mji huu unapoadhibiwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kunako mapambazuko, malaika wakawahimiza Loti, wakamwambia, “Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walioko hapa, la sivyo utaangamizwa wakati mji utakapoadhibiwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kunako mapambazuko, malaika wakamhimiza Lutu, wakamwambia, “Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walioko hapa, la sivyo utaangamizwa wakati mji utakapoadhibiwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, la sivyo utapotelea katika maangamizi ya mji huu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulipokucha, malaika wakamhimiza Loti wakisema, “Amka, mchukue mkeo na hawa binti zako wawili msije mkaangamia wakati mji huu unapoadhibiwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulipopambazuka, wale malaika wakamhimiza Loti kwamba: Ondoka! Mchukue mkeo nao wanao wawili wa kike, ulio nao, usiuawe nawe kwa ajili ya manza za mji huu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulipokucha, wamalaika wakamusihi Loti wakisema: “Amuka, utwae muke wako na hawa wabinti zako wawili musipate kuangamia wakati muji huu unapoazibiwa.”