Genesis 19:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Loti akawa anasitasita. Lakini kwa vile Mwenyezi-Mungu alivyomhurumia Loti, wale malaika wakamshika yeye, mkewe na binti zake wawili, wakamtoa nje ya mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipositasita, wale wanaume wakamshika mkono wake, na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwahurumia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Loti akawa anasitasita. Lakini kwa vile Mwenyezi-Mungu alivyomhurumia Loti, wale malaika wakamshika yeye, mkewe na binti zake wawili, wakamtoa nje ya mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa BWANA alikuwa na huruma kwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa bwana alikuwa na huruma kwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akakawiakawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mikono ya binti zake wawili, kwa jinsi BWANA alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Loti akawa anasitasita. Lakini kwa vile Mwenyezi-Mungu alivyomhurumia Loti, wale malaika wakamshika yeye, mkewe na binti zake wawili, wakamtoa nje ya mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipozuzuika, wale waume wakawashika mikono, yeye na mkewe na wanawe, kwa huruma, Bwana alizowapatia, wakawatoa mjini na kuwapeleka nje.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi BWANA alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Loti akakuwa anasitasita. Lakini kwa vile Yawe alivyomuhurumia Loti, wale wamalaika wakamushika yeye, muke wake na wabinti zake wawili, wakamutosha inje ya muji.