Genesis 19:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipowatoa nje ya mji, malaika mmoja wao akawaambia, “Kimbieni kwa usalama wenu. Msiangalie nyuma wala kusimama popote bondeni. Kimbilieni milimani, msije mkaangamia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja wao akawaambia, “Mkimbie kwa usalama wenu! Msitazame nyuma, wala msisimame popote katika nchi tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo mtaangamizwa!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipowatoa nje ya mji, malaika mmoja wao akawaambia, “Kimbieni kwa usalama wenu. Msiangalie nyuma wala kusimama popote bondeni. Kimbilieni milimani, msije mkaangamia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja wao akawaambia, “Mkimbie kwa usalama wenu! Msitazame nyuma, wala msisimame po pote katika tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo mtaangamizwa!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja wao akawaambia, “Mkimbie kwa usalama wenu! Msitazame nyuma, wala msisimame popote katika nchi tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo mtaangamizwa!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde popote; ujiponye mlimani, usije ukaangamia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipowatoa nje ya mji, malaika mmoja wao akawaambia, “Kimbieni kwa usalama wenu. Msiangalie nyuma wala kusimama popote bondeni. Kimbilieni milimani, msije mkaangamia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwisha kuwatoa na kuwapeleka nje, akasema: Iponye roho yako! Usitazame nyuma, wala usisimame huku bondeni mahali pawapo pote, ila kimbilia milimani, usiuawe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipowatosha inje ya muji, malaika mumoja wao akawaambia: “Mukimbie kwa ajili ya usalama wenu. Musiangalie nyuma wala kusimama popote katika bonde. Mukimbilie kwenye milima, musipate kuangamia.”