Genesis 19:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Mwenyezi-Mungu akateremsha moto mkali wa kiberiti kutoka mbinguni juu ya Sodoma na Gomora,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mwenyezi Mungu akanyesha moto wa kiberiti juu ya Sodoma na Gomora kutoka kwake Mwenyezi Mungu mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Mwenyezi-Mungu akateremsha moto mkali wa kiberiti kutoka mbinguni juu ya Sodoma na Gomora,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo BWANA akanyesha moto wa kiberiti juu ya Sodoma na Gomora, uliotoka mbinguni kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo bwana akanyesha moto wa kiberiti uliotoka mbinguni kwa bwana juu ya Sodoma na Gomora.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto kutoka mbinguni kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Mwenyezi-Mungu akateremsha moto mkali wa kiberiti kutoka mbinguni juu ya Sodoma na Gomora,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana aliponyesha mvua ya moto uliochanganyika na mawe ya kiberitiberiti kwenye miji ya Sodomu na Gomora; mvua hii ilitoka kwake Bwana mbinguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yawe akateremusha moto mukali wa kiberiti kutoka mbinguni juu ya Sodoma na Gomora,