Genesis 19:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu alipoiangamiza miji ya bondeni alimokuwa anakaa Loti, alimkumbuka Abrahamu kwa kumtoa Loti katika miji hiyo, ili Loti asije akaangamia pamoja nayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Mungu alipoiangamiza miji ya tambarare, alimkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu kutoka lile janga lililoharibu miji ile ambamo Lutu alikuwa ameishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu alipoiangamiza miji ya bondeni alimokuwa anakaa Loti, alimkumbuka Abrahamu kwa kumtoa Loti katika miji hiyo, ili Loti asije akaangamia pamoja nayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Mungu alipoiangamiza miji ya tambarare alimkumbuka Abrahamu, akamtoa Loti kutoka kwenye lile janga lililoharibu miji ile ambamo Loti alikuwa ameishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Mungu alipoiangamiza miji ya tambarare alimkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu kutoka kwenye lile janga lililoharibu miji ile ambamo Lutu alikuwa ameishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Abrahamu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu alipoiangamiza miji ya bondeni alimokuwa anakaa Loti, alimkumbuka Abrahamu kwa kumtoa Loti katika miji hiyo, ili Loti asije akaangamia pamoja nayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hapo, Mungu alipoiangamiza miji ya lile bonde, Mungu alimkumbuka Aburahamu, amtoe Loti katika mafudikizo hayo na kumpeleka pengine alipoifudikiza hiyo miji, Loti alimokuwa na kukaa humo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu alipoangamiza miji katika bonde ambamo Loti alikuwa anakaa, alimukumbuka Abrahamu kwa kumutosha Loti katika miji hiyo, kusudi Loti asiangamizwe pamoja nayo.