Genesis 19:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamwita Loti na kumwuliza, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako? Watoe nje. Tunataka kulala nao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamwita Lutu wakisema, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuwalawiti.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamwita Loti na kumwuliza, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako? Watoe nje. Tunataka kulala nao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamwita Loti wakisema, “Wako wapi wale watu ambao walikuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuweze kuwalawiti.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamwita Lutu wakisema, “Wako wapi wale watu ambao walikuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuweze kuwalawiti.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wako wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwalete kwetu, ili tuweze kuwajua kimwili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamwita Loti na kumwuliza, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako? Watoe nje. Tunataka kulala nao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakamwita Loti, wakamwuliza: Wako wapi wale waume waliokuja kwako usiku huu? Walete, watutokee, tupate kuwajua!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamwita Loti na kumwuliza: “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako? Uwatoshe inje. Tunataka kulala nao.”