Genesis 19:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wao wakasema, “Tupishe! Wewe ulikuja huku ukiwa mgeni na sasa wajifanya hakimu! Basi, tutakutenda mabaya zaidi ya hao wageni wako.” Hapo wakamsukuma Loti nyuma hata karibu wauvunje mlango wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamjibu, “Tuondokee mbali!” Wakaendelea kusema, “Huyu mtu alikuja hapa kama mgeni na sasa anataka kuwa mwamuzi wetu! Tutakutenda vibaya kuliko wao.” Waliendelea kumlazimisha Lutu na kuusogelea mlango ili kuuvunja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wao wakasema, “Tupishe! Wewe ulikuja huku ukiwa mgeni na sasa wajifanya hakimu! Basi, tutakutenda mabaya zaidi ya hao wageni wako.” Hapo wakamsukuma Loti nyuma hata karibu wauvunje mlango wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamjibu, “Tuondokee mbali.” Wakaendelea kusema, “Huyu mtu alikuja hapa kama mgeni na sasa anataka kuwa mwamuzi wetu! Tutakutenda vibaya kuliko wao.” Waliendelea kumlazimisha Loti na kusonga mbele ili kuvunja mlango.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamjibu, “Tuondokee mbali.” Wakaendelea kusema, “Huyu mtu alikuja hapa kama mgeni na sasa anataka kuwa mwamuzi wetu! Tutakutenda vibaya kuliko wao.” Waliendelea kumlazimisha Lutu na kusonga mbele ili kuvunja mlango.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakasema, “Ondoka hapa!” Kisha wakasema, “Mtu huyu amekuja kukaa kwetu kama mgeni; naye kumbe anataka kuhukumu! Basi tutakutenda vibaya kuliko hawa”. Wakamsonga sana Lutu, wakakaribia wauvunje mlango.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wao wakasema, “Tupishe! Wewe ulikuja huku ukiwa mgeni na sasa wajifanya hakimu! Basi, tutakutenda mabaya zaidi ya hao wageni wako.” Hapo wakamsukuma Loti nyuma hata karibu wauvunje mlango wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakasema: Ondoka hapa! Tena wakaambiana: Ni mgeni peke yake kwetu, tena anataka kutuamua. Wakamsonga sana huyu Loti wakitaka kuukaribia mlango, wauvunje.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wao wakasema: “Utupitishe! Wewe ulikuja huku ukiwa mugeni na sasa unajifanya kuwa mwamuzi! Basi, tutakutendea mabaya zaidi ya wale wageni wako.” Halafu wakamusukuma Loti nyuma hata karibu wavunje mulango wake.