Genesis 2:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kutoka katika udongo, Mwenyezi-Mungu akaumba kila mnyama wa porini na kila ndege wa angani, halafu akamletea huyo mwanamume aone atawapa majina gani; na majina aliyowapa viumbe hao, yakawa ndio majina yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa ametengeneza kutoka ardhi wanyama pori wote, na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa jina lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kutoka katika udongo, Mwenyezi-Mungu akaumba kila mnyama wa porini na kila ndege wa angani, halafu akamletea huyo mwanamume aone atawapa majina gani; na majina aliyowapa viumbe hao, yakawa ndio majina yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi BWANA Mungu alikuwa amefanyiza kutoka katika ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lo lote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi bwana Mwenyezi Mungu alikuwa amefanyiza kutoka ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kutoka katika udongo, Mwenyezi-Mungu akaumba kila mnyama wa porini na kila ndege wa angani, halafu akamletea huyo mwanamume aone atawapa majina gani; na majina aliyowapa viumbe hao, yakawa ndio majina yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu alipokwisha kuwatokeza katika nchi nyama wote wa porini na ndege wote wa angani akawapeleka kwa Adamu, aone, atakavyowaita; jina lake kila nyama mwenye uzima liwe lilo hilo, Adamu atakalomwita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yawe akaumba kutoka udongo kila nyama wa pori na kila ndege wa anga, halafu akamuletea yule mwanaume aone atawapa majina gani. Na majina aliyowapa viumbe hao, yakakuwa ndiyo majina yao.