Genesis 2:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya ndio maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa. Bwana Mwenyezi Mungu alipoziumba mbingu na dunia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa. BWANA Mungu alipoziumba mbingu na dunia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa. bwana Mwenyezi Mungu alipoziumba mbingu na dunia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilivyoumbwa. Siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na nchi
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo ndivyo, mbingu na nchi zilivyopata kuwapo hapo, zilipoumbwa. Siku hizo, Bwana Mungu alipozifanya nchi na mbingu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na nchi
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa. Siku ile Yawe Mungu alipoumba mbingu na dunia,