Genesis 2:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hapakuwa na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwa na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kuilima ardhi,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa BWANA Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana BWANA Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
miti yote ya mashambani ilikuwa haijawa bado, nazo mboga zote za mashambani zilikuwa hazijaota bado, kwa kuwa Bwana Mungu alikuwa hajanyesha bado mvua katika nchi, tena hakuwako mtu wa kulima shamba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana BWANA Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
hakukukuwa mimea juu ya inchi wala miti haikukuwa imeota maana Yawe Mungu hakukuwa ameinyeshea inchi mvua, wala hakukukuwa mutu wa kuilima.