Genesis 20:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo, kwa kweli, yeye ni dada yangu: Baba yake na baba yangu ni mmoja, lakini mama tofauti; ndiyo maana akawa mke wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti ya baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye kweli ni ndugu yangu, binti wa baba yangu ila siye mwana wa mama yangu, ndipo akawa mke wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo, kwa kweli, yeye ni dada yangu: baba yake na baba yangu ni mmoja, lakini mama tofauti; ndiyo maana akawa mke wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata hivyo, kwa kweli yeye ni dada yangu, yaani binti wa baba yangu na wala sio binti wa mama yangu; ndipo akawa mke wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo, kwa kweli, yeye ni dada yangu: Baba yake na baba yangu ni mmoja, lakini mama tofauti; ndiyo maana akawa mke wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye ni dada yangu kweli kwa kuwa mwana wa baba yangu, lakini si mwana wa mama yangu, kwa hiyo aliweza kuwa mke wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye kweli ni ndugu yangu, binti wa baba yangu ila siye mwana wa mama yangu, ndipo akawa mke wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaidi ya hayo, kwa kweli, yeye ni dada yangu: baba yake na baba yangu ni mumoja, lakini mama tofauti; ndiyo maana aliweza kuwa muke wangu.