Genesis 20:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akiwa huko, Abrahamu alisema kuwa mkewe Sara ni dada yake. Kwa hiyo, mfalme Abimeleki wa Gerari akamchukua Sara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huko Ibrahimu akasema kuhusu Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu.” Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akaagiza Sara aletwe, naye akamchukua awe mkewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akiwa huko, Abrahamu alisema kuwa mkewe Sara ni dada yake. Kwa hiyo, mfalme Abimeleki wa Gerari akamchukua Sara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
huko Abrahamu akasema kuhusu Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu.” Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma Sara aletwe, naye akamchukua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
huko Ibrahimu akasema kuhusu Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu.” Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma Sara aletwe, naye akamchukua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Abrahamu akanena juu ya Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu”. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wakamtwaa Sara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akiwa huko, Abrahamu alisema kuwa mkewe Sara ni dada yake. Kwa hiyo, mfalme Abimeleki wa Gerari akamchukua Sara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa ajili ya mkewe Sara Aburahamu akasema: Huyu ni dada yangu. Kwa hiyo Abimeleki, mfalme wa Gerari, akatuma watu kumchukua Sara.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akiwa kule, Abrahamu alisema kwamba muke wake Sara ni dada yake. Kwa hiyo, mufalme Abimeleki wa Gerari akamutwaa Sara.