Genesis 20:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abrahamu mwenyewe ndiye aliyesema kuwa huyu ni dada yake. Tena hata Sara mwenyewe alisema kuwa Abrahamu ni kaka yake! Mimi nimefanya nilivyofanya kwa moyo mnyofu na sina hatia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu’; naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri safi na mikono safi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na mwanamke mwenyewe naye alisema, Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kuwa safi mikono yangu, nimefanya hivi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abrahamu mwenyewe ndiye aliyesema kuwa huyu ni dada yake. Tena hata Sara mwenyewe alisema kuwa Abrahamu ni kaka yake! Mimi nimefanya nilivyofanya kwa moyo mnyofu na sina hatia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu,’ naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri njema na mikono safi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu,’ naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri njema na mikono safi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Hukuniambia mwenyewe, “Huyu ni dada yangu?” Na mwanamke mwenyewe naye akasema, “Huyu ni kaka yangu”. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kutojua kwangu, nimefanya hivi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abrahamu mwenyewe ndiye aliyesema kuwa huyu ni dada yake. Tena hata Sara mwenyewe alisema kuwa Abrahamu ni kaka yake! Mimi nimefanya nilivyofanya kwa moyo mnyofu na sina hatia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule hakuniambia: Huyu ni dada yangu? Naye mwenyewe amesema: Yule ni kaka yangu. Hivyo nimevifanya kwa moyo usiojua kuwa vibaya na kwa mikono iliyotakata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na mwanamke mwenyewe naye alisema, Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kuwa safi mikono yangu, nimefanya hivi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Si ni Abrahamu mwenyewe ndiye aliyesema kwamba huyu ni dada yake? Tena hata Sara mwenyewe alisema kwamba Abrahamu ni kaka yake! Mimi nimefanya nilivyofanya kwa moyo safi na sina kosa.”