Genesis 21:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mungu akamwambia Abrahamu, “Usihuzunike kwa sababu ya mtoto huyu, wala huyo mtumwa wako wa kike. Lolote akuambialo Sara lifanye; kwa kweli wazawa wako watatokana na Isaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana huyo na mjakazi wako. Sikiliza lolote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mungu akamwambia Abrahamu, “Usihuzunike kwa sababu ya mtoto huyu, wala huyo mtumwa wako wa kike. Lolote akuambialo Sara lifanye; kwa kweli wazawa wako watatokana na Isaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana na mtumishi wako wa kike. Sikiliza lo lote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia Isaki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana na mtumishi wako wa kike. Sikiliza lolote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu akamwambia Abrahamu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mungu akamwambia Abrahamu, “Usihuzunike kwa sababu ya mtoto huyu, wala huyo mtumwa wako wa kike. Lolote akuambialo Sara lifanye; kwa kweli wazawa wako watatokana na Isaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini Mungu akamwambia Aburahamu: Neno hilo lisiwe baya machoni pako kwa ajili ya huyo kijana na huyo kijakazi wako! Yote, Sara atakayokuambia, mwitikie sauti yake! Kwani watakaoitwa uzao wako ni wa Isaka tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Mungu akamwambia Abrahamu: “Usihuzunike kwa sababu ya mutoto huyu, wala huyo mujakazi wako. Jambo lolote Sara atakalokuambia ulifanye. Maana ni kwa njia ya Isaka utapata wazao watakaoitwa wako.