Genesis 21:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari na kumtwika begani; akamfukuza pamoja na mwanawe. Hagari akaondoka, akawa anatangatanga nyikani Beer-sheba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kesho yake asubuhi na mapema, Ibrahimu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hajiri. Akaviweka begani mwa Hajiri, akamwondoa pamoja na kijana. Hajiri akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari na kumtwika begani; akamfukuza pamoja na mwanawe. Hagari akaondoka, akawa anatangatanga nyikani Beer-sheba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kesho yake asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari. Akaviweka mabegani mwa Hagari, akamwondoa pamoja na kijana. Akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kesho yake asubuhi na mapema, Ibrahimu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari. Akaviweka mabegani mwa Hagari, akamwondoa pamoja na kijana. Hagari akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Abrahamu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akamtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari na kumtwika begani; akamfukuza pamoja na mwanawe. Hagari akaondoka, akawa anatangatanga nyikani Beer-sheba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake Aburahamu akaamka na mapema, akachukua mkate na kibuyu cha maji, akampagaza Hagari begani, kisha akampa na mwanawe; ndivyo, alivyompa ruhusa kwenda zake. Lakini alipokwenda akapotea katika nyika ya Beri-Seba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo, asubui mapema, Abrahamu akatwaa chakula na chupa la maji, akamupa Hagari na kumubebesha mutoto juu ya bega. Akamufukuza pamoja na mwana wake. Hagari akaondoka, akakuwa anatangatanga katika jangwa la Beri-Seba.