Genesis 22:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malaika akamwambia, “Usimdhuru mtoto wala usimfanye lolote! Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwani hukuninyima hata mwanao wa pekee.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malaika akamwambia, “Usimdhuru mtoto wala usimfanye lolote! Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwani hukuninyima hata mwanao wa pekee.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lo lote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, kwa kuwa hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malaika akamwambia, “Usimdhuru mtoto wala usimfanye lolote! Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwani hukuninyima hata mwanao wa pekee.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwambia: Usimkunjulie mtoto mkono wako! Usimfanyizie cho chote! Kwani sasa nimejua, ya kuwa unamwogopa Mungu, maana hukumnyima hata mwanao wa pekee.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika akamwambia: “Usinyooshe mukono wako juu ya kijana wala usimufanyie jambo lolote! Sasa ninajua kwamba unamwogopa Mungu, maana haukuninyima hata mwana wako wa pekee.”