Genesis 22:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
hakika nitakubariki, na wazawa wako nitawazidisha kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ufuoni mwa bahari. Wazawa wako wataimiliki miji ya adui zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga wa pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
hakika nitakubariki, na wazawa wako nitawazidisha kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ufuoni mwa bahari. Wazawa wako wataimiliki miji ya adui zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hakika, nitakubariki na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
hakika nitakubariki, na wazawa wako nitawazidisha kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ufuoni mwa bahari. Wazawa wako wataimiliki miji ya adui zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nitakubariki kweli, nikupe, uzao wako uwe watu wengi sana kama nyota za mbinguni au kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari, hao wa uzao wako wayatwae malango ya adui zao kuwa yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
hakika nitakubariki, na wazao wako nitawazidisha kama nyota mbinguni na kama muchanga pembeni ya bahari. Wazao wako watarizi miji ya waadui zao.