Genesis 22:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Abrahamu akawarudia wale watumishi wake, nao kwa pamoja wakaondoka, wakarudi Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Ibrahimu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wote, wakaenda hadi Beer-Sheba. Naye Ibrahimu akaishi huko Beer-Sheba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Abrahamu akawarudia wale watumishi wake, nao kwa pamoja wakaondoka, wakarudi Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Abrahamu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wakaenda wote pamoja mpaka Beer-Sheba. Abrahamu akaishi huko Beer-Sheba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Ibrahimu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wakaenda wote pamoja mpaka Beer-Sheba. Ibrahimu akaishi huko Beer-Sheba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Abrahamu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Abrahamu akawarudia wale watumishi wake, nao kwa pamoja wakaondoka, wakarudi Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Aburahamu akarudi kwa wale vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja kwenda Beri-Seba; kule Beri-Seba ndiko, Aburahamu alikokaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Abrahamu akawarudilia wale watumishi wake, nao pamoja wakaondoka, wakarudi Beri-Seba. Abrahamu akakaa kule Beri-Seba.