Genesis 22:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Isaka akamwuliza baba yake, “Baba, moto na kuni tunazo; lakini mwanakondoo wa sadaka ya kuteketezwa yuko wapi?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isaka akamwambia Ibrahimu baba yake, “Baba yangu!” Ibrahimu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.” Isaka akasema, “Moto na kuni zipo. Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Isaka akamwuliza baba yake, “Baba, moto na kuni tunazo; lakini mwanakondoo wa sadaka ya kuteketezwa yuko wapi?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, “Baba yangu!” Abrahamu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.” Isaki akasema, “Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isaka akanena akamwambia Ibrahimu baba yake, “Baba yangu!” Ibrahimu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.” Isaka akasema, “Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Isaka akasema na Abrahamu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Isaka akamwuliza baba yake, “Baba, moto na kuni tunazo; lakini mwanakondoo wa sadaka ya kuteketezwa yuko wapi?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Isaka akamwmbia baba yake Aburahamu: Baba! Akajibu: Mimi hapa, mwanangu! Akasema: Tazama! Moto na kuni tunazo, lakini mwana kondoo wa kuwa ng'ombe ya tambiko yuko wapi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Isaka akamwuliza baba yake: “Baba, tuko na moto na kuni. Lakini mwana-kondoo wa sadaka ya kuteketezwa yuko wapi?”