Genesis 23:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abrahamu akakubaliana na Efroni, akampimia kiasi cha fedha alichotaja mbele ya Wahiti wote, fedha shekeli 400, kadiri ya vipimo vya wafanyabiashara wa wakati huo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ibrahimu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: shekeli mia nne za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ibrahimu akakubali maneno ya Efroni. Ibrahimu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abrahamu akakubaliana na Efroni, akampimia kiasi cha fedha alichotaja mbele ya Wahiti wote, fedha shekeli 400, kadiri ya vipimo vya wafanyabiashara wa wakati huo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Abrahamu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: Shekeli 400 za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ibrahimu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: Shekeli 400 za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Abrahamu akakubali maneno ya Efroni. Abrahamu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abrahamu akakubaliana na Efroni, akampimia kiasi cha fedha alichotaja mbele ya Wahiti wote, fedha shekeli 400, kadiri ya vipimo vya wafanyabiashara wa wakati huo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aburahamu akamwitikia Efuroni; kwa hiyo Aburahamu akampimia Efuroni hizo fedha, alizozisema masikioni pao wana wa Hiti, fedha 400, wachuuzi walizozitumia, ndio shilingi 1600.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ibrahimu akakubali maneno ya Efroni. Ibrahimu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abrahamu akakubaliana na Efuroni, akamupimia kadiri ya feza alizotaja mbele ya Wahiti wote, feza vikoroti mia ine, kadiri ya vipimo vya wachuuzi wa wakati ule.