Genesis 24:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, huyo mtumishi akachukua ngamia kumi wa bwana wake akaondoka akiwa na zawadi nzuri za kila aina. Akasafiri kwenda katika mji alimokaa Nahori, nchini Mesopotamia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo huyo mtumishi akachukua ngamia kumi miongoni mwa ngamia wa bwana wake, akaondoka, akiwa amechukua aina zote za vitu vizuri kutoka kwa bwana wake. Akaelekea Mesopotamia, akaenda hadi mji wa Nahori.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha huyo mtumishi akatwaa ngamia kumi katika ngamia za bwana wake akaenda zake, maana mali zote za bwana wake zilikuwa mkononi mwake, akaondoka, akaja mpaka Mesopotamia, mpaka mji wa Nahori.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, huyo mtumishi akachukua ngamia kumi wa bwana wake akaondoka akiwa na zawadi nzuri za kila aina. Akasafiri kwenda katika mji alimokaa Nahori, nchini Mesopotamia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo huyo mtumishi akachukua ngamia kumi miongoni mwa ngamia za bwana wake akaondoka, akachukua aina zote za vitu vizuri kutoka kwa bwana wake. Akaelekea Aramu-Naharaimu na kushika njia kwenda mji wa Nahori.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo huyo mtumishi akachukua ngamia kumi miongoni mwa ngamia za bwana wake, akaondoka, akiwa amechukua aina zote za vitu vizuri kutoka kwa bwana wake. Akaelekea Aramu-Naharaimu na kushika njia kwenda mji wa Nahori.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha huyo mtumishi akatwaa ngamia kumi katika ngamia za bwana wake akaenda zake, maana mali zote za bwana wake zilikuwa mkononi mwake, akaondoka, akaja mpaka Mesopotamia, mpaka mji wa Nahori.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, huyo mtumishi akachukua ngamia kumi wa bwana wake akaondoka akiwa na zawadi nzuri za kila aina. Akasafiri kwenda katika mji alimokaa Nahori, nchini Mesopotamia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha yule mtumishi akachukua ngamia kumi za bwana wake kwenda safari, akachukua navyo vitu vizuri vyote vya bwana wake, kisha akaondoka, akaenda Mesopotamia kwenye mji wa Nahori.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha huyo mtumishi akatwaa ngamia kumi katika ngamia za bwana wake akaenda zake, maana mali zote za bwana wake zilikuwa mkononi mwake, akaondoka, akaja mpaka Mesopotamia, mpaka mji wa Nahori.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, yule mutumishi akatwaa ngamia kumi wa bwana wake akaondoka akiwa na zawadi nzuri za kila aina. Akasafiri kwenda katika muji Nahori alimokaa, katika inchi ya Mesopotamia.