Genesis 24:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mtu akawa anamtazama kwa makini bila kusema lolote, apate kufahamu kama Mwenyezi-Mungu ameifanikisha safari yake au sivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pasipo kusema neno, yule mtumishi akamtazama kwa makini aone kama Mwenyezi Mungu ameifanikisha safari yake, au la.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi yule mtu akamkazia macho, akanyamaza, ili ajue kwamba Bwana ameifanikisha safari yake ama sivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mtu akawa anamtazama kwa makini bila kusema lolote, apate kufahamu kama Mwenyezi-Mungu ameifanikisha safari yake au sivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pasipo kusema neno, yule mtumishi akamtazama kwa makini aone kama BWANA ameifanikisha safari yake, au la.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pasipo kusema neno, yule mtumishi akamtazama kwa makini aone kama bwana ameifanikisha safari yake, au la.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi yule mtu akamkazia macho, akanyamaza, ili ajue kama BWANA ameifanikisha safari yake ama sivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mtu akawa anamtazama kwa makini bila kusema lolote, apate kufahamu kama Mwenyezi-Mungu ameifanikisha safari yake au sivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mtu akamstaajabu, lakini akanyamaza, apate kujua, kama Bwana amemtimizia vema safari yake, au kama sivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi yule mtu akamkazia macho, akanyamaza, ili ajue kwamba BWANA ameifanikisha safari yake ama sivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mutu akakuwa anamwangalia kwa uangalifu bila kusema lolote, apate kufahamu kama Yawe amefanikisha safari yake au sivyo.