Genesis 24:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ngamia walipotosheka kunywa maji, yule mtu akampa huyo msichana pete ya dhahabu yenye uzito upatao gramu sita, na bangili mbili za dhahabu za gramu kumi kila moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikawa ngamia walipokwisha kunywa wote, yule mtumishi akampa huyo msichana pete ya puani ya dhahabu yenye uzito wa beka moja, na bangili mbili za dhahabu zenye uzito wa shekeli kumi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ngamia walipotosheka kunywa maji, yule mtu akampa huyo msichana pete ya dhahabu yenye uzito upatao gramu sita, na bangili mbili za dhahabu za gramu kumi kila moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa ngamia walipokwisha kunywa wote, yule mtumishi akampa huyo msichana pete ya puani ya dhahabu yenye uzito wa beka moja na bangili mbili za dhahabu zenye uzito wa shekeli kumi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikawa ngamia walipokwisha kunywa wote, yule mtumishi akampa huyo msichana pete ya puani ya dhahabu yenye uzito wa beka moja na bangili mbili za dhahabu zenye uzito wa shekeli kumi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ngamia walipotosheka kunywa maji, yule mtu akampa huyo msichana pete ya dhahabu yenye uzito upatao gramu sita, na bangili mbili za dhahabu za gramu kumi kila moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ngamia walipokwisha kunywa wote, yule mtu akatoa pete la dhahabu lenye uzito kama wa shilingi na vikuku viwili vya dhahabu vyenye uzito wa sekeli kumi, ndio robo ya ratli, akamtia mikononi pake,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ngamia walipotosheka kunywa maji, yule mutu akamupa yule binti pete ya zahabu yenye uzito wa yapata grama sita, na vikomo viwili vya zahabu za grama kumi kila moja.