Genesis 24:32 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mtumishi huyo wa Abrahamu akaingia nyumbani. Labani akawafungua ngamia na kuwapatia majani ngamia wake, akampa yeye na watu wake maji ya kunawa miguu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo yule mtumishi akaingia nyumbani, nayo mizigo ikaondolewa juu ya ngamia. Majani na malisho yakaletwa kwa ajili ya ngamia, na maji kwa ajili yake na watu wake ili kunawa miguu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mtu yule akaingia katika nyumba, akawafungua ngamia; naye akatoa majani na malisho kwa ngamia, na maji ya kuoshea miguu yake, na miguu ya watu waliokuwa pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mtumishi huyo wa Abrahamu akaingia nyumbani. Labani akawafungua ngamia na kuwapatia majani ngamia wake, akampa yeye na watu wake maji ya kunawa miguu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo yule mtumishi akaenda nyumbani, mizigo ikaondolewa juu ya ngamia. Majani na malisho yakaletwa kwa ajili ya ngamia na maji kwa ajili yake na watu wake ili kunawa miguu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo yule mtumishi akaenda nyumbani, mizigo ikaondolewa juu ya ngamia. Majani na malisho yakaletwa kwa ajili ya ngamia na maji kwa ajili yake na watu wake ili kunawa miguu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mtu yule akaingia katika nyumba, akawafungua ngamia; naye akatoa majani na malisho kwa ngamia, na maji ya kuoshea miguu yake, na miguu ya watu waliokuwa pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mtumishi huyo wa Abrahamu akaingia nyumbani. Labani akawafungua ngamia na kuwapatia majani ngamia wake, akampa yeye na watu wake maji ya kunawa miguu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mtu alipoingia nyumbani, huyu akawafungua ngamia mizigo yao, akawapa mabua ya kulalia na majani ya kulisha, naye mwenyewe akampa maji ya kuiosha miguu yake nayo miguu ya watu waliokuwa naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mtu yule akaingia katika nyumba, akawafungua ngamia; naye akatoa majani na malisho kwa ngamia, na maji ya kuoshea miguu yake, na miguu ya watu waliokuwa pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mutumishi yule wa Abrahamu akaingia ndani ya nyumba. Labani akafungua ngamia na kuwapatia majani, akamupa yeye na watu wake maji ya kunawa miguu.