Genesis 24:40 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini yeye akasema, ‘Mwenyezi-Mungu aniongozaye maishani mwangu, atamtuma malaika wake aende pamoja nawe na kukufanikisha katika safari yako; nawe utamtwalia mwanangu mke kutoka kwa jamaa yangu na nyumba ya baba yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Akanijibu, ‘Mwenyezi Mungu, ambaye nimetembea mbele zake, atatuma malaika wake pamoja nawe, na kuifanikisha safari yako, ili uweze kupata mke kwa ajili ya mwanangu katika ukoo wangu na kutoka jamaa ya baba yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaniambia, Bwana, ambaye naenenda machoni pake, atapeleka malaika wake pamoja nawe, atafanikisha njia yako; nawe umtwalie mwanangu mke katika jamaa zangu, na wa nyumba ya babangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini yeye akasema, ‘Mwenyezi-Mungu aniongozaye maishani mwangu, atamtuma malaika wake aende pamoja nawe na kukufanikisha katika safari yako; nawe utamtwalia mwanangu mke kutoka kwa jamaa yangu na nyumba ya baba yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Akanijibu, ‘BWANA ambaye nimetembea mbele zake, atatuma malaika wake pamoja nawe, na kuifanikisha safari yako, ili uweze kupata mke kwa ajili ya mwanangu katika ukoo wangu na kutoka katika jamaa ya baba yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Akanijibu, ‘ bwana ambaye nimetembea mbele zake, atatuma malaika wake pamoja nawe, na kuifanikisha safari yako, ili uweze kupata mke kwa ajili ya mwanangu katika ukoo wangu na kutoka jamaa ya baba yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaniambia, BWANA, ambaye naenenda machoni pake, atatuma malaika wake pamoja nawe, atafanikisha njia yako; nawe umtwalie mwanangu mke katika jamaa zangu, na wa nyumba ya babangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini yeye akasema, ‘Mwenyezi-Mungu aniongozaye maishani mwangu, atamtuma malaika wake aende pamoja nawe na kukufanikisha katika safari yako; nawe utamtwalia mwanangu mke kutoka kwa jamaa yangu na nyumba ya baba yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, aliponiambia: Bwana, ambaye ninafanya mwenendo machoni pake, atatuma malaika wake kwenda na wewe, akupe, safari yako ifanikiwe, umposee mwanangu mke kwao ndugu zangu waliomo nyumbani mwa baba yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaniambia, BWANA, ambaye naenenda machoni pake, atapeleka malaika wake pamoja nawe, atafanikisha njia yako; nawe umtwalie mwanangu mke katika jamaa zangu, na wa nyumba ya babangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini yeye akasema: ‘Yawe aliyeniongoza katika maisha yangu, atamutuma malaika wake aende pamoja nawe na kukufanikisha katika safari yako. Nawe utamutwalia mwana wangu muke kutoka kwa jamaa yangu na nyumba ya baba yangu.