Genesis 24:41 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama utakapofika kwa jamaa zangu hawatakupa huyo msichana, basi, hutafungwa na kiapo changu.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha, utakapoenda kwenye ukoo wangu, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu. Hata wakikataa kukupa huyo binti, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo utafunguliwa kiapo changu hapo utakapowafikilia jamaa zangu; nao wasipokupa msichana huyo, utafunguliwa kiapo changu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama utakapofika kwa jamaa zangu hawatakupa huyo msichana, basi, hutafungwa na kiapo changu.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha, utakapokwenda kwenye ukoo wangu, utakuwa umefunguliwa kutoka katika kiapo changu hata kama wakikataa kukupa huyo binti, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha, utakapokwenda kwenye ukoo wangu, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu hata kama wakikataa kukupa huyo binti, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo utafunguliwa kiapo changu hapo utakapowafikia jamaa zangu; hata wasipokupa msichana huyo, utafunguliwa kiapo changu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama utakapofika kwa jamaa zangu hawatakupa huyo msichana, basi, hutafungwa na kiapo changu.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo utakapofika kwa ndugu zangu utakuwa uemfunguliwa, nacho kiapo, ninachokutakia, kitakuwa kimetanguka; usipompata kwao, utakuwa umefunguliwa kweli, nacho kiapo, ninachokutakia, kitakuwa kimetanguka kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo utafunguliwa kiapo changu hapo utakapowafikilia jamaa zangu; nao wasipokupa msichana huyo, utafunguliwa kiapo changu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utakapofika kwa jamaa yangu, nao wasipokupa yule binti, basi, hautafungwa na kiapo changu.’