Genesis 24:44 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
naye akanipa na kuwatekea maji ngamia wangu, basi huyo na awe ndiye uliyemchagua kuwa mke wa mwana wa bwana wangu.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye akiniambia, “Kunywa, nami nitawatekea ngamia wako maji pia,” basi huyo awe ndiye mke Mwenyezi Mungu amemchagulia mwana wa bwana wangu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye akaniambia, Unywe wewe, na ngamia zako pia nitawatekea, huyo na awe ndiye mke Bwana aliyemwekea mwana wa bwana wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
naye akanipa na kuwatekea maji ngamia wangu, basi huyo na awe ndiye uliyemchagua kuwa mke wa mwana wa bwana wangu.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye kama akiniambia, “Kunywa, nami nitateka maji kwa ajili ya ngamia wako pia,” basi huyo awe ndiye mke ambaye BWANA amemchagulia mwana wa bwana wangu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye kama akiniambia, “Kunywa, nami nitateka maji kwa ajili ya ngamia wako pia,” basi huyo awe ndiye mke ambaye bwana amemchagulia mwana wa bwana wangu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naye akaniambia, Unywe wewe, na ngamia wako pia nitawatekea, huyo na awe ndiye mke BWANA aliyemwekea mwana wa bwana wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
naye akanipa na kuwatekea maji ngamia wangu, basi huyo na awe ndiye uliyemchagua kuwa mke wa mwana wa bwana wangu.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
naye akiniambia: Haya! Unywe wewe mwenyewe! nao ngamia wako nitawachotea, basi, awe yeye mwanamke, Bwana aliyemchagulia mwana wa bwana wangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye akaniambia, Unywe wewe, na ngamia zako pia nitawatekea, huyo na awe ndiye mke BWANA aliyemwekea mwana wa bwana wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
naye akinipa na kuwatekea ngamia wangu maji, basi yule akuwe ndiye uliyemuchagua kuwa muke wa mwana wa bwana wangu.’