Genesis 24:45 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, mara Rebeka alifika na mtungi wake wa maji begani, akateremka kisimani na kuteka maji. Nami nikamwambia, ‘Tafadhali nipe maji ya kunywa.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, Rebeka akatokea, na mtungi begani mwake. Akashuka kisimani, akateka maji, nami nikamwambia, ‘Tafadhali nipe maji ninywe.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata kabla sijaisha kusema moyoni mwangu, tazama! Rebeka akatokea, na mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka. Nami nikamwambia, Tafadhali nipe maji ninywe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, mara Rebeka alifika na mtungi wake wa maji begani, akateremka kisimani na kuteka maji. Nami nikamwambia, ‘Tafadhali nipe maji ya kunywa.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, Rebeka akatokea, amebeba mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka maji, nami nikamwambia, ‘Tafadhali unipe maji ninywe.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, Rebeka akatokea, amebeba mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka maji, nami nikamwambia, ‘Tafadhali nipe maji ninywe.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata kabla sijaisha kusema moyoni mwangu, tazama! Rebeka akatokea, na mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka. Nami nikamwambia, Tafadhali nipe maji ninywe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, mara Rebeka alifika na mtungi wake wa maji begani, akateremka kisimani na kuteka maji. Nami nikamwambia, ‘Tafadhali nipe maji ya kunywa.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nilipokuwa sijaisha bado kuyasema moyoni mwangu, mara nikamwona Rebeka, akitokea mwenye mtungi wake begani pake, akashuka kisimani kuchota. Ndipo, nilipomwambia: Nipe maji, ninywe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata kabla sijaisha kusema moyoni mwangu, tazama! Rebeka akatokea, na mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka. Nami nikamwambia, Tafadhali nipe maji ninywe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mbele sijamaliza kuomba ndani ya moyo wangu, mara tu Rebeka akafika na mutungi wake wa maji juu ya bega, akateremuka kwenye kisima na kuteka maji. Nami nikamwambia: ‘Tafazali unipe maji ya kunywa.’