Genesis 24:46 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akautua mtungi wake haraka kutoka begani mwake, akasema, ‘Haya, kunywa bwana wangu. Nitawatekea maji ngamia wako pia.’ Basi mimi nikanywa na ngamia wangu pia akawapa maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Akafanya haraka kushusha mtungi wake begani na kusema, ‘Kunywa, na nitawanywesha ngamia wako pia.’ Basi nikanywa, naye akawanywesha na ngamia pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akafanya haraka akatua mtungi wake chini, akanena, Unywe, na ngamia zako nitawanywesha pia; basi nikanywa, akawanywesha na ngamia nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akautua mtungi wake haraka kutoka begani mwake, akasema, ‘Haya, kunywa bwana wangu. Nitawatekea maji ngamia wako pia.’ Basi mimi nikanywa na ngamia wangu pia akawapa maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Akafanya haraka kushusha mtungi wake begani na kusema, ‘Kunywa na nitawanywesha ngamia wako pia,’ basi nikanywa, akawanywesha na ngamia pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Akafanya haraka kushusha mtungi wake begani na kusema, ‘Kunywa na nitawanywesha ngamia wako pia,’ basi nikanywa, akawanywesha na ngamia pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akafanya haraka akatua mtungi wake chini, akasema, Unywe, na ngamia wako nitawanywesha pia; basi nikanywa, akawanywesha na ngamia nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akautua mtungi wake haraka kutoka begani mwake, akasema, ‘Haya, kunywa bwana wangu. Nitawatekea maji ngamia wako pia.’ Basi mimi nikanywa na ngamia wangu pia akawapa maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akaushusha upesi mtungi wake toka begani, akasema: Haya! Unywe! Nao ngamia wako nitawapa, wanywe. Nilipokwisha kunywa, akawanywesha ngamia nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akafanya haraka akatua mtungi wake chini, akanena, Unywe, na ngamia zako nitawanywesha pia; basi nikanywa, akawanywesha na ngamia nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akatua mutungi wake haraka toka juu ya bega lake, akasema: ‘Basi, kunywa bwana wangu. Nitatekea ngamia wako maji vilevile.’ Basi, mimi nikakunywa naye akawapa ngamia wangu maji vilevile.