Genesis 24:54 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtumishi wa Abrahamu na watu aliokuja nao wakala, wakanywa na kulala huko. Walipoamka asubuhi, mtumishi yule akasema, “Naomba kurudi kwa bwana wangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha yeye na wale watu waliokuwa pamoja naye wakala, wakanywa na kulala palepale. Walipoamka asubuhi, yule mtumishi akasema, “Nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakala wakanywa, yeye na watu waliokuwa pamoja naye, nao wakakaa usiku. Wakaondoka asubuhi, naye akasema, Nipeni ruhusa niende kwa bwana wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtumishi wa Abrahamu na watu aliokuja nao wakala, wakanywa na kulala huko. Walipoamka asubuhi, mtumishi yule akasema, “Naomba kurudi kwa bwana wangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha yeye na wale watu waliokuwa pamoja naye wakala, wakanywa na kulala pale pale. Walipoamka asubuhi, yule mtumishi, akasema, “Nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha yeye na wale watu waliokuwa pamoja naye wakala, wakanywa na kulala palepale. Walipoamka asubuhi, yule mtumishi, akasema, “Nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakala, wakanywa, yeye na watu waliokuwa pamoja naye, nao wakakaa usiku. Wakaondoka asubuhi, naye akasema, Nipeni ruhusa niende kwa bwana wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtumishi wa Abrahamu na watu aliokuja nao wakala, wakanywa na kulala huko. Walipoamka asubuhi, mtumishi yule akasema, “Naomba kurudi kwa bwana wangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakala, wakanywa yeye nao wale watu waliokuwa naye, kisha wakalala. Asubuhi walipoamka, akawaambia: Nipeni ruhusa kwenda kwa bwana wangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakala wakanywa, yeye na watu waliokuwa pamoja naye, nao wakakaa usiku. Wakaondoka asubuhi, naye akasema, Nipeni ruhusa niende kwa bwana wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutumishi wa Abrahamu na watu aliokuja nao wakakula, wakakunywa na kulala kule. Walipoamuka asubui, mutumishi yule akasema: “Ninaomba kurudi kwa bwana wangu.”