Genesis 24:60 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakambariki Rebeka wakisema, “Ewe dada yetu! Uwe mama wa maelfu kwa maelfu; wazawa wako waimiliki miji ya adui zao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakambariki Rebeka, wakamwambia, “Ndugu yetu, uwe wewe kumi elfu, mara elfu nyingi; nao wazao wako wamiliki malango ya adui zao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakambarikia Rebeka, wakamwambia, Ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakambariki Rebeka wakisema, “Ewe dada yetu! Uwe mama wa maelfu kwa maelfu; wazawa wako waimiliki miji ya adui zao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakambariki Rebeka, wakamwambia, “Ndugu yetu, uwe wewe kumi elfu, mara elfu nyingi, nao wazao wako wamiliki malango ya adui zao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakambariki Rebeka, wakamwambia, “Ndugu yetu, uwe wewe kumi elfu, mara elfu nyingi, nao wazao wako wamiliki malango ya adui zao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakambariki Rebeka, wakamwambia, Dada yetu, wewe uwe mama wa elfu kumi, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakambariki Rebeka wakisema, “Ewe dada yetu! Uwe mama wa maelfu kwa maelfu; wazawa wako waimiliki miji ya adui zao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakambariki Rebeka, wakamwambia: Ndugu yetu, na uwe mama ya maelfu na maelfu! Nao wa uzao wako na wayakalie malango ya adui zao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakambarikia Rebeka, wakamwambia, Ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wakamubariki Rebeka wakisema: “Ewe dada yetu! Ukuwe mama wa maelfu kwa maelfu; wazao wako warizi miji ya waadui zao.”