Genesis 24:67 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Isaka akamchukua Rebeka ndani ya hema iliyokuwa ya Sara mama yake, akawa mke wake. Isaka akampenda Rebeka na kupata faraja baada ya kifo cha mama yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isaka akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake. Isaka akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaka akampenda; akafarijika baada ya kifo cha mama yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Isaka akamchukua Rebeka ndani ya hema iliyokuwa ya Sara mama yake, akawa mke wake. Isaka akampenda Rebeka na kupata faraja baada ya kifo cha mama yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Isaki akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake, Isaki akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaki akampenda, akafarijika baada ya kifo cha mama yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Isaka akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake, Isaka akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaka akampenda, akafarijika baada ya kifo cha mama yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mama yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Isaka akamchukua Rebeka ndani ya hema iliyokuwa ya Sara mama yake, akawa mke wake. Isaka akampenda Rebeka na kupata faraja baada ya kifo cha mama yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Isaka alipomwingiza Rebeka hemani mwa mama yake Sara, akamwoa, akawa mkewe, naye akampenda. Ndivyo Isaka alivyotulizwa moyo kwa ajili ya kufa kwa mama yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Isaka akamutwaa Rebeka ndani ya hema iliyokuwa ya mama yake Sara, naye akakuwa muke wake. Isaka akamupenda Rebeka na kupata kufarijika nyuma ya kifo cha mama yake.