Genesis 25:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ishmaeli alikuwa na umri wa miaka 137 alipofariki, akajiunga na wazee wake waliotangulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa jumla Ishmaeli aliishi miaka mia moja na thelathini na saba (137). Akapumua pumzi ya mwisho, akafa, naye akakusanywa pamoja na watu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hii ndiyo miaka ya maisha ya Ishmaeli, miaka mia na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ishmaeli alikuwa na umri wa miaka 137 alipofariki, akajiunga na wazee wake waliotangulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa jumla Ishmaeli aliishi miaka 137. Akapumua pumzi ya mwisho, akafa, naye akakusanywa pamoja na watu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa jumla Ishmaeli aliishi miaka 137. Akapumua pumzi ya mwisho, akafa, naye akakusanywa pamoja na watu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ishmaeli aliishi miaka mia moja na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ishmaeli alikuwa na umri wa miaka 137 alipofariki, akajiunga na wazee wake waliotangulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo hii ndiyo miaka ya kuwapo kwake Isimaeli, miaka 137; kisha akazimia, akafa, akachukuliwa kwenda kwao walio wa ukoo wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hii ndiyo miaka ya maisha ya Ishmaeli, miaka mia na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Isimaeli alikuwa na umri wa miaka mia moja makumi tatu na saba alipokufa na kukutana na wazee wake.