Genesis 25:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Mataifa mawili yamo tumboni mwako; makabila mawili yatakayozaliwa nawe, yatafarakana. Moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine; mkubwa atamtumikia mdogo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akamjibu, “Mataifa mawili yamo tumboni mwako, na mataifa hayo mawili kutoka ndani yako watatenganishwa. Mmoja atakuwa na nguvu kuliko mwingine, na yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamwambia,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Mataifa mawili yamo tumboni mwako; makabila mawili yatakayozaliwa nawe, yatafarakana. Moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine; mkubwa atamtumikia mdogo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akamjibu, “Mataifa mawili yamo tumboni mwako, na mataifa hayo mawili kutoka ndani yako watatenganishwa, mmoja atakuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine, na mkubwa atamtumikia mdogo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akamjibu, “Mataifa mawili yamo tumboni mwako, na mataifa hayo mawili kutoka ndani yako watatenganishwa. Mmoja atakuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine, na yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamwambia, Mataifa mawili yako tumboni mwako, Na makabila mawili ya watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Mataifa mawili yamo tumboni mwako; makabila mawili yatakayozaliwa nawe, yatafarakana. Moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine; mkubwa atamtumikia mdogo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akamwambia: Mataifa mawili yamo tumboni mwako, kabila mbili za watu zinatengana tumboni mwako zikitaka kutoka, kabila moja itatenda nguvu kuishinda ile nyingine, naye mkubwa atamtumikia nduguye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamwambia, Mataifa mawili yako tumboni mwako, Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akamwambia: “Mataifa mawili yako ndani ya tumbo lako; makabila mawili yatakayozaliwa nawe, yatatengana. Moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine, mukubwa atamutumikia mudogo.”