Genesis 25:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja, Yakobo alipokuwa anapika dengu, Esau alirudi nyumbani kutoka mawindoni ana njaa sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku moja Yakobo alipika mchuzi wa dengu. Esau akarudi kutoka porini akiwa na njaa kali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja, Yakobo alipokuwa anapika dengu, Esau alirudi nyumbani kutoka mawindoni ana njaa sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku moja Yakobo alipika mchuzi wa dengu, Esau akarudi kutoka porini akiwa na njaa kali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku moja Yakobo alipika mchuzi wa dengu, Esau akarudi kutoka porini akiwa na njaa kali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka mbugani, naye alikuwa amechoka sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja, Yakobo alipokuwa anapika dengu, Esau alirudi nyumbani kutoka mawindoni ana njaa sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku moja Yakobo alipopika kunde, Esau akarudi toka porini, naye alikuwa amechoka sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja, Yakobo alipokuwa anapika muchuzi, Esau akarudi kwa nyumba kutoka katika mawindo akiwa na njaa sana.