Genesis 25:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watoto wa kiume wa masuria wake akawapa zawadi, na wakati alipokuwa bado hai, aliwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka mwanawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Ibrahimu alipokuwa bado hai, akawapa watoto wa masuria wake zawadi, kisha akawaondoa waende kuishi pande za mashariki mbali na mwanawe Isaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watoto wa kiume wa masuria wake akawapa zawadi, na wakati alipokuwa bado hai, aliwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka mwanawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini alipokuwa bado hai, akawapa watoto wa masuria wake zawadi kisha akawaondoa waende kuishi pande za mashariki mbali na mwanawe Isaki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Ibrahimu alipokuwa bado hai, akawapa watoto wa masuria wake zawadi, kisha akawaondoa waende kuishi pande za mashariki mbali na mwanawe Isaka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Abrahamu, Abrahamu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watoto wa kiume wa masuria wake akawapa zawadi, na wakati alipokuwa bado hai, aliwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka mwanawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wana wa masuria, Aburhamu aliokuwa nao, Aburahamu akawapa matunzo, kisha akawatuma angaliko mzima kuondoka kwa mwanawe Isaka, waende upande wa maawioni kwa jua kukaa katika nchi ya huko maawioni kwa jua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini akawapa wana wa habara zake zawadi. Na wakati alipokuwa bado muzima, akawapeleka katika inchi ya upande wa mashariki, mbali na mwana wake Isaka.