Genesis 26:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Isaka akavichimbua vile visima vilivyokuwa vimechimbwa wakati Abrahamu baba yake alipokuwa hai, visima ambavyo Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kifo cha Abrahamu. Akavipa majina yaleyale aliyovipa baba yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Isaka akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Ibrahimu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya Ibrahimu kufa, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Isaka akavichimbua vile visima vilivyokuwa vimechimbwa wakati Abrahamu baba yake alipokuwa hai, visima ambavyo Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kifo cha Abrahamu. Akavipa majina yaleyale aliyovipa baba yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Isaki akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Abrahamu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Abrahamu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Isaka akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Ibrahimu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Ibrahimu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Abrahamu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Abrahamu; naye akaviita majina kufuata majina aliyoviita babaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Isaka akavichimbua vile visima vilivyokuwa vimechimbwa wakati Abrahamu baba yake alipokuwa hai, visima ambavyo Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kifo cha Abrahamu. Akavipa majina yaleyale aliyovipa baba yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipovirudia na kuvichimbua tena vile visima vya maji, walivyovichimbua siku zile za baba yake Aburahamu, Wafilisti walivyoviziba, Aburahamu alipokwisha kufa, akaviita majina yaleyale, baba yake aliyoviita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Isaka akachimba vile visima vilivyokuwa vimechimbwa wakati Abrahamu baba yake alipokuwa muzima, visima ambavyo Wafilistini walikuwa wameziba nyuma ya kifo cha Abrahamu. Akavipa majina yaleyale baba yake aliyovipa.