Genesis 26:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usiku huohuo Mwenyezi-Mungu alimtokea na kumwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako Abrahamu. Usiogope kwa kuwa niko pamoja nawe; nitakubariki na kuwazidisha wazawa wako kwa ajili ya Abrahamu, mtumishi wangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Usiku ule Mwenyezi Mungu akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Ibrahimu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe. Nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usiku huohuo Mwenyezi-Mungu alimtokea na kumwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako Abrahamu. Usiogope kwa kuwa niko pamoja nawe; nitakubariki na kuwazidisha wazawa wako kwa ajili ya Abrahamu, mtumishi wangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Usiku ule BWANA akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Abrahamu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe, nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Usiku ule bwana akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Ibrahimu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe, nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Abrahamu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubariki, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usiku huohuo Mwenyezi-Mungu alimtokea na kumwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako Abrahamu. Usiogope kwa kuwa niko pamoja nawe; nitakubariki na kuwazidisha wazawa wako kwa ajili ya Abrahamu, mtumishi wangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko Bwana akamtokea usiku uleule, akamwambia: Mimi ni Mungu wa baba yako Aburahamu; usiogope! Kwani mimi niko pamoja na wewe, nikubariki na kuwafanya wao wa uzao wako kuwa wengi kwa ajili ya mtumishi wangu Aburahamu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usiku uleule Yawe alimutokea na kumwambia: “Mimi ni Mungu wa baba yako Abrahamu. Usiogope; niko pamoja nawe. Nitakubariki na kuwazidisha wazao wako kwa ajili ya Abrahamu, mutumishi wangu.”