Genesis 26:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake wakaamka asubuhi na mapema na kula kiapo. Kisha Isaka akawasindikiza na kuagana nao kwa amani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kesho yake asubuhi na mapema wakaapiana. Kisha Isaka akawaruhusu waende zao, wakamwacha kwa amani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaapiana wao kwa wao, kisha Isaka akawapa ruhusa, nao wakaenda zao kwa amani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake wakaamka asubuhi na mapema na kula kiapo. Kisha Isaka akawasindikiza na kuagana nao kwa amani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kesho yake asubuhi na mapema, wakaapizana wao kwa wao. Kisha Isaki akawaruhusu waende zao, wakamwacha Isaki kwa amani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kesho yake asubuhi na mapema, wakaapizana wao kwa wao. Kisha Isaka akawaruhusu waende zao, wakamwacha Isaka kwa amani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaapiana wao kwa wao, kisha Isaka akawapa ruhusa, nao wakaenda zao kwa amani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake wakaamka asubuhi na mapema na kula kiapo. Kisha Isaka akawasindikiza na kuagana nao kwa amani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake wakaamka na mapema, wakaapiana kila mmoja na mwenziwe, kisha Isaka akawasindikiza, wakitoka kwake kwenda zao na kutengemana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaapiana wao kwa wao, kisha Isaka akawapa ruhusa, nao wakaenda zao kwa amani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake wakaamuka asubui mapema na kufanya kiapo. Kisha Isaka akawasindikiza na kuagana nao kwa amani.