Genesis 26:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa huko walipomwuliza habari za mkewe, yeye alijibu, “Huyu ni dada yangu.” Aliogopa kusema kwamba ni mke wake kwa kuogopa kwamba wakazi wa nchi wangemuua kwa sababu ya Rebeka, maana Rebeka alikuwa mzuri sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanaume wa mahali pale walipomuuliza habari za mke wake, akasema, “Huyu ni dada yangu,” kwa sababu aliogopa kusema, “Huyu ni mke wangu.” Alifikiri, “Wanaume wa huku wanaweza kuniua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa ni mzuri wa sura.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa huko walipomwuliza habari za mkewe, yeye alijibu, “Huyu ni dada yangu”; aliogopa kusema kwamba ni mke wake kwa kuogopa kwamba wakazi wa nchi wangemuua kwa sababu ya Rebeka, maana Rebeka alikuwa mzuri sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa mahali pale walipomwuliza habari za mke wake, akasema, “Huyu ni dada yangu,” kwa sababu aliogopa kusema, “Huyu ni mke wangu.” Alifikiri, “Watu wa mahali pale wataweza kumwua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa alikuwa mzuri wa sura.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa mahali pale walipomuuliza habari za mke wake, akasema, “Huyu ni dada yangu,” kwa sababu aliogopa kusema, “Huyu ni mke wangu.” Alifikiri, “Watu wa mahali pale wataweza kumuua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa alikuwa mzuri wa sura.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni dada yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa huko walipomwuliza habari za mkewe, yeye alijibu, “Huyu ni dada yangu.” Aliogopa kusema kwamba ni mke wake kwa kuogopa kwamba wakazi wa nchi wangemuua kwa sababu ya Rebeka, maana Rebeka alikuwa mzuri sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nao waume wa mahalai hapo walipomwuliza habari ya mkewe, akasema: Huyu ni dada yangu, kwani aliogopa kusema: Ni mke wangu, kwa kwamba: Waume wa mahali hapa wasije kuniua kwa ajili ya Rebeka, kwani ni mzuri wa kumtazama.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa kule walipomwuliza juu ya muke wake, akajibu: “Huyu ni dada yangu.” Aliogopa kusema kwamba ni muke wake kwa kuogopa kwamba wakaaji wa inchi wangemwua kwa sababu ya Rebeka, maana Rebeka alikuwa muzuri sana.