Genesis 27:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Isaka alikuwa amezeeka na macho yake yalikuwa hayaoni. Basi, alimwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu!” Naye akaitika “Naam baba, nasikiliza!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isaka alipokuwa mzee na macho yake yakapofuka kwa kukosa nguvu, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu.” Akajibu, “Mimi hapa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Isaka alikuwa amezeeka na macho yake yalikuwa hayaoni. Basi, alimwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu!” Naye akaitika “Naam baba, nasikiliza!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Isaki alipokuwa mzee na macho yake yalipokuwa yamekosa nguvu asiweze kuona tena, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu.” Akajibu, “Mimi hapa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isaka alipokuwa mzee na macho yake yalipokuwa yamekosa nguvu asiweze kuona tena, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu.” Akajibu, “Mimi hapa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Isaka alikuwa amezeeka na macho yake yalikuwa hayaoni. Basi, alimwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu!” Naye akaitika “Naam baba, nasikiliza!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, Isaka alipokuwa mkongwe, macho yake yakatenda kiza, yasione; ndipo, alipomwita mwanawe mkubwa Esau, akamwambia: Mwanangu! Naye akamwitikia: Mimi hapa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ilikuwa wakati Isaka alipokuwa muzee na macho yake yalikuwa zaifu hata hakuweza kuona tena, akaita Esau mwana wake mukubwa, akamwambia: “Mwana wangu!” Naye akaitika: “Niko hapa!”